
KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA AZAM FC FULL MKOKO
KIKOSI cha Yanga dhidi ya Azam FC ni full mkoko katika mchezo wa nusu fainali Kombe la Mapinduzi
KIKOSI cha Yanga dhidi ya Azam FC ni full mkoko katika mchezo wa nusu fainali Kombe la Mapinduzi
JEREMIA Kisubi, kipa namba tatu wa Simba leo Januari 10,2022 ametambulishwa ndani ya kikosi cha Mtibwa Sugar. Usajili wake ni wa mkopo akitokea Simba ambapo huko alikuwa hapati nafasi ya kuanza katika mechi za ushindani. Aliibuka ndani ya Simba akitokea Tanzania Prisons ambapo huko alikuwa ni chaguo namba moja la benchi la ufundi. Ni…
MTAMBO wa mabao ndani ya kikosi cha Yanga umeanza kazi kwa ajili ya kuivutia kasi Azam FC kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi unaotarajiwa kuchezwa leo. Januari 10,2022 Yanga ambao ni mabingwa watetezi wana kazi ya kusaka ushindi mbele ya Azam FC kwenye mchezo wa nusu fainali unaotarajiwa kuchezwa saa 10:15. Fiston…
PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wanahitaji kulitwaa Kombe la Mapinduzi hivyo leo watapambana kupata matokeo mbele ya Namungo FC. Saa 2:15 usiku Simba itakuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya Namungo FC kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali. Mshindi wa mchezo wa leo atakutana na mshindi wa mchezo wa nusu…
LEO Jumatatu, Januari 10,2022 inatarajiwa kuchezwa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar ambapo mechi mbili zinatarajiwa kuchezwa. Ni mabingwa watetezi wa taji hilo ambao ni Yanga wao watamenyana na Azam FC itakuwa ni saa 10:15 jioni. Mchezo mwingine ni ule wa pili ambao utazikutanisha Simba v Namungo, itakuwa ni saa 2:15 usiku. Washindi kwenye…
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Championi Jumatatu
TAARIFA zinasema kwamba, Kiungo Mshambuliaji wa Yanga, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ amefuatwa nyumbani kwao Burundi na viongozi wa timu moja kutoka Uarabuni kwa ajili ya mazungumzo ili kumsajili. Saido ambaye hivi karibuni aliondoka Tanzania kwenda Burundi kwa ajili ya mapumziko mafupi, wakati akiwa huko ndipo Waarabu hao walipomuibukia kwa nia ya kumshawishi wamsajili. Nyota huyo aliyetua Yanga dirisha dogo la msimu uliopita, mkataba wake unatarajiwa kumalizikamwisho wa msimu huu. Mtu wa…
KUELEKEA katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi kesho Januari 10 kati ya Yanga dhidi ya Azam FC baadhi ya nyota wanatarajiwa kuukosa mchezo huo kutokana na sababu mbalimbali. Yanga ni mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi ambapo waliweza kulitwaa taji hilo kwa ushindi wa penalti mbele ya Simba. Ni Salum Aboubakhari, ‘SureBoy’ ambaye ni kiungo…
PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wachagua kuwapa furaha mashabiki wa timu hiyo hivyo kesho watafanya vizuri kusaka ushindi. Januari 10 Simba itakuwa na kibarua kwenye Kombe la Mapinduzi ambapo inatarajia kumenyana na Namungo FC kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali. Mchezo wake uliopita ilitoshana nguvu na Mlandege na dakika 90 zilikamilika…
IMEFAHAMIKA kuwa uongozi wa Yanga umetumia Sh 50 Mil kufanikisha usajili wa mshambuliaji wa Mbeya Kwanza, Chrispin Ngushi aliyekuwa akiwindwa pia na Simba na kumpa mkataba wa miaka mitatu. Usajili wa Ngushi mwenye mabao matatu akicheza michezo 11 ya Ligi Kuu Bara msimu huu, ni wa nne kwa Yanga kusajiliwa kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo uliofunguliwa Desemba 16, 2021. Wachezaji wengine waliosajiliwa na Yanga na kutambulishwa ni Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ kutoka Azam…
ABDULKARIM Amin,’Popat’ Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Azam FC amesema kuwa wanatambua kwamba mchezo wao wa kesho dhidi ya Yanga utakuwa na ushindani mkubwa lakini wamejipanga kusaka ushindi. Kesho Januari 10 Yanga inatarajiwa kucheza na Azam FC kwenye mchezo wa nusu fainali Kombe la Mapinduzi. Yanga ni mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi na mchezo…
NYOTA wapya wa timu ya Yanga ambao wametua ndani ya dirisha dogo, wameipa jeuri timu hiyo kiasi cha kutamka kuwa wana uhakika wa kutetea ubingwa wao wa Kombe la Mapinduzi. Mabosi hao wameongeza kuwa wana uhakika huo kwa mastaa hao wapya ndani ya kikosi hicho, wakiamini wana uwezo mkubwa. Miongoni mwa mastaa wapya ambao wamesajiliwa na Yanga ni Dennis Nkane aliyetoka Biashara United, Aboutwalib Mshery, Salim Aboubakhari ‘Sure Boy’ na Crispin Ngushi. Yanga ni mabingwa watetezi na mchezo wa kwanza mbele ya…
OFISA Habari wa Azam FC, Zakaria Zakazi amesema kuwa mchezo uliopita walifungwa mabao 2-0 katika mchezo wa ligi sasa wanakwenda kukutana kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi watapambana kufanya vizuri na yule ambaye atakuwa na mpango mzuri atapata matokeo mazuri na utapigwa mchezo mkubwa.
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Spoti Xtra Jumapili, nakala yake ni jero
SIMBA Queens imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Yanga Princess katika mchezo wa Ligi ya Wanawake. Mchezo huo umechezwa leo Januari 8, Uwanja wa Mkapa na Simba Queens imesepa na pointi zote tatu. Mchezo ujao utakuwa ni wa mzunguko wa pili na unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mo Simba Arena.
KWENYE mchezo wa Kombe la Mapinduzi kati ya Simba v Mlandenge ambapo baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Amaan, Januari 7 ulisoma Mlandege 0-0 Simba. Mchezaji bora alichaguliwa kuwa ni Hassan Abdallah na alipewa zawadi na NIC ya shilingi laki tano ameweka wazi kuwa walijipanga kushinda ila ilikuwa tofauti kutokana na uimara wa…
KITU pekee ambacho mashabiki wa Simba na Yanga wanakifurahia kwa sasa ni kuziona timu hizo zikiendelea kukipiga kwenye Kombe la Mapinduzi licha ya kubanwa kwenye mechi zao za mwisho za makundi. Vigogo hao wa soka bara licha ya kuwa na sehemu kubwa ya vikosi vyao lakini walishindwa kuzibeba pointi tatu kwenye mechi hizo za mwisho ambapo waliambulia pointi moja tu. Yanga ndiyo walikuwa wa kwanza kucheza ambapo walitoshana…