SAID Ntibanzokiza, aliyekuwa nyota wa kikosi cha Yanga anatajwa kuibukia ndani ya kikosi cha Singida Big Stars ambayo zamani ilikuwa inaitwa DTB.
Timu hiyo imepanda Ligi Kuu Bara msimu huu wa 2021/22 ikitokea Championship na msimu ujao wa 2022/23 itakuwa ndani ya ligi.
Habari zimeeleza kuwa timu hiyo ambayo itakuwa na maskani yake Singida huku ikitumia Uwanja wa Liti kwa mechi za nyumbani imefanya mazungumzo na mchezaji huyo.
Saido aliachwa na Yanga rasmi Mei 30 baada ya mkataba wake wa miaka miwili kumeguka.
Hivyo nyota huyo ataibuka Singida akiwa ni mchezaji huru na ataendelea kuwa ndani ya ligi ikiwa dili lake litafanikiwa.
Nyota huyo mchezo wake wa mwisho kucheza ndani ya Yanga ilikuwa dhidi ya Biashara United uliokamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.
SAN SEBASTIÁN, 17/12/2023.- El delantero nigeriano de la Real Sociedad Sadiq Umar (c) disputa un balón con el defensa hispano marroquí del Betis Chadi Riad (d) durante el encuentro entre Real Sociedad y Betis correspondiente a la jornada 17 de LaLiga Santander, este domingo en el Reale Arena de San Sebastián. EFE/ Javier Etxezarreta