Home Sports KOMBE LA DUNIA NDANI YA TANZANIA

KOMBE LA DUNIA NDANI YA TANZANIA

KOMBE la Dunia kwa sasa lipo kwenye ardhi ya Tanzania, Dar ndipo linapatikana kwa sasa.

Hii ni desturi ya Shirikisho la Soka la Kimataifa, (Fifa) huwa wanakuwa na desturi ya kulitembeza Kombe la Dunia ambalo kwa mwaka 2022 linatarajiwa kuanza Novemba 21 hadi Desemba 18 huko Qatar.

 Jana Mei 31 Rais wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu, aliweza kulipokea na kufanya hafla fupi na iliyofana iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Leo Juni Mosi litakuwa Uwanja wa Mkapa ambapo Watanzania watapata fursa ya kupiga nalo picha kombe hilo pamoja na mataifa mengine bila shaka kwa kuwa Tanzania inashirikiana vema na mataifa yote.

Ni nyota wa zamani wa Barcelona na Chelsea, Juliano Belleti ndiye anayeoongoza ziara ya kombe hilo kuja Tanzania aliwahi kubeba taji hilo mwaka 2002 akiwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Brazil.

Ikumbukwe kwamba taji hili kubwa la dunia ni dhahabu tupu lilianza kufanyika mwaka 1930.

Previous articleSIMBA YAFANYA KIKAO NA KOCHA MPYA SAA 72
Next articleNTIBANZOKIZA ATAJWA KUIBUKIA SINGIDA BIG STARS