Home Sports KOCHA BENCHIKHA OUT SIMBA

KOCHA BENCHIKHA OUT SIMBA

KOCHA Abdelhakh Benchikha aliyekuwa akiifundisha Simba sasa hatakuwa katikakatika majukumu hayo baada ya makubaliano ya pande zote mbili.

Benchikha mrithi wa mikoba ya Robert Oliveira mchezomchezo wake wa kwanza Kariakoo Dabi ilikuwa Aprili 20 2024 ubao ulisoma Yanga 2-1 Simba.

Ni yeye alikuwa na timu katika mashindano ya Muungano 2024 kwenye mechi mbili walishinda zote na kutwaa taji hilo.

Taarifa iliyotolewa na Simba imeeleza kuwa wamefikia makubaliano ya kuachana na Benchikha pamoja na wasaidizi wake ambapo Benchikha ana matatizo ya kifamilia.

Timu itakuwa chini ya Juma Mgunda na Seleman Matola ambaye ni msaidizi mchezo ujao kwa Simba mabingwa wa Muungano 2024 itakuwa dhidi ya Namungo, Aprili 30 Uwanja wa Majaliwa.

Previous articleJKT TANZANIA KWENYE KAZI NYINGINE TENA
Next articleMeridianbet Expanse Tournament Unashinda Maokoto Huku Unatabasamu