Home Sports BENCHIKHA MALENGO ILIKUWA UBINGWA AFRIKA

BENCHIKHA MALENGO ILIKUWA UBINGWA AFRIKA

KOCHA Abdelhakh Benchikha, kocha wa kazi amesema kuwa malengo makubwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika ilikuwa ni kucheza hatua ya nusu fainali na kutwaa ubingwa lakini ilishindikana kwa kuwa haikuwa mipango ya Mungu.

Aprili 28 2024 Simba ilitoa taarifa rasmi kuwa wamefikia makubaliano ya pande mbili kuvunja mkataba kati ya Simba na kocha Benchikha pamoja na Wasaidizi wake wawili Kamal Boujnam na Farid Zemit.

Sababu ya Benchikha kuomba mkataba uvunjwe ni matatizo ya kifamilia yanayomkabili nyumbani kwao Algeria na sasa timu ya Simba itakuwa chini ya Juma Mgunda na Seleman Matola hadi hapo Bodi ya Wakurugenzi itakapotoa uamuzi mwingine.

Benchikha amesema:” Malengo katika Ligi ya Mabingwa Afrika ilikuwa ni kuona kwamba tunafika hatua ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa Afrika lakini haikuwa mipango ya Mungu.

“Tumeondolewa na Al Ahly hii sio timu ndogo ni timu kubwa ambayo inafanya vizuri, kitaifa na kimataifa, “.

Mchezo wa kwanza kwa Juma Mgunda na Matola unatarajiwa kuchezwa Aprili 30 itakuwa dhidi ya Namungo.

Previous articleALIYEKUWA ANAPIGIWA HESABU SIMBA AMALIZANA NA YANGA
Next articleMERIDIANBET YATOA MSAADA WA NGUO ZA KUJIKINGA NA MVUA KWA MADEREVA BODABODA NA BAJAJI, WAFANYABIASHARA DAR