Home Sports YANGA YATUMA UJUMBE HUU BAADA YA PABLO KUCHIMBISHWA

YANGA YATUMA UJUMBE HUU BAADA YA PABLO KUCHIMBISHWA

BAADA ya Klabu ya Simba kutangaza kuvunja mkataba na kocha wake mkuu, Pablo Franco, Raia wa Hispania, Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amesema kuwa ni moja ya makocha wenye nidhamu.

Pablo alisaini dili la miaka miwili kutumika ndani ya Simba na alitua Bongo Novemba 10,2021 na mchezo wake wa kwanza alishinda mabao 3-1 dhidi ya Ruvu Shooting.

Kocha huyo mchezo wake wa mwisho kukaa kwenye benchi ilikuwa mbele ya Yanga ambapo alipoteza kwa kufungwa bao 1-0 lililofungwa na Feisal Salum.

Manara amesema:“Kocha Bora mwenye nidhamu kubwa na mapenzi mazito na football pamoja na wachezaji wake anaondoka nchini. Pamoja na kufanya kazi katika mazingiza magumu ya kukosa Proper Management iliyogubikwa na migogoro isiyoisha, jamaa aliiwezesha Club yake kufika  Robo Fainali ya Shirikisho.

“Binafsi nitam-miss, (kumbuka) kwa uungwana wake na ucheshi wake. Kila la kheri rafiki yangu Pablo. Kwa msimu huu tu wewe ni kocha wa pili kufukuzwa na naamini hadi msimu uishe tutasikia mengi,” amesema Manara.

Previous articleHUYU HAPA KOCHA MPYA SIMBA
Next articleJEMBE HILI LA KAZI NYIA NYEUPE KUTUA SIMBA