DEMBELE AKATWA MKWANJA HUKO KISA DAKIKA TATU
OUSMANE Dembele, nyota wa kikosi cha Barcelona amekuwa wa kwanza kukutana na balaa la kocha mpya, Xavi Hernandez kisa kuchelewa kwenye mazoezi kwa muda wa dakika tatu pekee. Kwa kosa hilo ambalo amefanya amekutana na ishu ya kukatwa mkwanja mrefu kwenye mshahara wake hivyo asitarajie kupewa mshahara wake kamili kwa mwezi huu kwa kuwa amesharikoroga…