BOXER BADO UNA MUDA WAKURUDI TENA KATIKA UBORA

    Zama za Mwinyi Zahera alikuwa katika ubora na aliaminika kikosi cha kwanza jumlajumla ni Paul Godfrey wengi wanapenda kumuita Boxer..

    Aliweza kumuweka benchi Juma Abdul mzee wa kumwaga maji ambaye pia alikuwa ni nahodha msaidizi katika kikosi cha Yanga.

    Majeruhi yaliweza kuirudisha nyuma kasi yake kisha hata aliporudi hajaweza kurudi kwenye ule ubora.

    Alipata nafasi katika Kombe la Mapinduzi mwaka 2022 bado alikuwa katika kazi ya kujitafuta na Yanga ilikwama kutetea taji ikatolewa na Azam FC kwa penalti 9-8.

    Bado muda upo wa kuweza kurudi tena katika ubora kwa kuongeza juhudi na nidhamu katika kazi.

    Bado taifa linahitaji ule ubora usiochuja katika kupeperusha bendera ya Tanzania inawezekana na inawezekana.

    Hajawa na nafasi katika mechi za Ligi Kuu Bara msimu huu wa 2021/22 kutokana na ushindani wa namba lakini anaweza kupenya ikiwa ataongeza juhudi.

    Previous articleMAYELE LIMEMKUTA JAMBO HUKO
    Next articleUWANJA WA MKAPA NGOMA NZITO SIMBA 0-0 PRISONS