USAJILI UFANYWE KWA UMAKINI MKUBWA

  ILIKUWA ni Desemba 16 baada ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa na sasa ni Januari 6 mambo yanazidi kwenda kasi huku vurugu za usajili zikiendelea.

  Ule usemi wa mwenye kisu kikali atakula nyama anayopenda inaendelea kwa sasa lakini ni lazima mipango iwe makini kwa kila timu.

  Iwe ni kwa timu ambazo zinashiriki Ligi Kuu Bara, Championship na Ligi ya Wanawake muda ni wao kuweza kufanya usajili kwa ajili ya timu zao.

  Ni mwaka mwingine tena kwa sasa tupo ambao ni 2022 ikiwa kila mmoja atafikiria kuendelea na mambo yale ya 2021 hapo lazima atafeli.

  Furaha ya kuupokea mwaka mpya iendane na kasi ya kila mmoja kutimiza majukumu yake kwa wakati kwa wale ambao hawana mpango wa kufanya usajili basi kikombe hiki kiwaepuke.

  Wapo wale ambao watafanya usajili kwa kufuata mahitaji yao hilo lipo wazi kwa kuwa ni mambo ambayo yapo kwenye soka letu na yanaumiza kwa kuwa lawama hupelekwa kwenye benchi.

  Kwa wakati huu uliobaki basi kila mmoja na atomize majukumu yake ili kuepuka lawama mwisho.

  Timu zote ambazo zitafanya usajili kwa mapendekezo yao binafsi wakati wa kujua masuala hayo yanakuja,  mchezo wa mpira hauhitaji mambo mengi zaidi ya vitendo.

  Muda wa kujua haya yote ni uwanjani kwani kuna wachezaji ambao walikuja kwa mbwembwe na nderemo lakini mwisho wa siku wakabuma.

  Kama atasajiliwa kwa presha wakati huu haina haja ya kuwa na haraka itafahamika tu pale wachezaji watakapokuwa wanacheza naye jina lake litaonekana mahali lilipo kama ni kikosi cha kwanza, benchi ama jukwaani.

  Wapo wachezaji wengine waliweza kupata nafasi ya kusajiliwa kwenye timu mpya lakini maisha yao kwenye ukurasa mpya yalikuwa nayo ni mapya.

  Hamna namna kila mchezaji anapenda kucheza lakini kama atashindwa kukidhi vigezo vya kocha basi atasubiri na mpaka muda ukifika basi atakuwa amejenga ushkaji mkubwa na benchi.

  Kila la kheri kwa wachezaji ambao watapata nafasi kwenye timu mpya na wale ambao wataongezewa mikataba yao jukumu lao ni moja kufanya kazi kwa juhudi.

  Tukiachana na timu na mchezaji pia ana kazi ya kuangalia nafasi yake kule anakokwenda asifikirie kupata mkwanja huku nafasi yake ya kucheza akiiweka kapuni itampoteza.

  Kwa kuwa maisha ya soka lazima yaendelee mchezaji mmoja kutoka na kwenda kwenye timu nyingine ni muda sahihi wa kila mchezaji ambaye anakwenda kuanza maisha mapya.

  Imani yangu ni kwamba mpaka pale dirisha la usajili litakapofungwa kila kitu kitakuwa kimekwenda sawa ndani ya timu zote kuanzia zile za Ligi Daraja la Kwanza, Daraja la Pili,Ligi ya Wanawake pamoja na zile zinazoshiriki Ligi Kuu Bara.

  Kila mtu atavuna kile atakachokipanda ndani ya uwanja ni wakati wa kuanza maandalizi kwa timu zote kwani muda wa ligi kuanza upo njiani na muda wa dirisha la usajili kufungwa upo karibu.

  Yote kwa yote wasisahau kwamba makosa makubwa ya timu kupata ushindi ni kwenye maandalizi na usajili hivyo wanapaswa kuwa bora katika usajili wakati huu ambao unaelekea ukingoni pamoja na kuanza maandalizi mapema kujenga timu zao.

  Muhimu ni kufanya maandalizi mazuri hasa kwa wachezaji ambao watasajiliwa kwa wakati huu. Jambo jingine ni kuweza kuwekeza kwa vijana wao ambao walipanda nao ili waweze kuwapa matokeo baadaye.

  Lakini licha ya kumaliza kufanya usajili mzuri ni muhimu kuwa na mpango kazi makini utakaofanya timu iwe inapata matokeo uwanjani na kuleta ushindani.

  Usajili mzuri ni ule ambao unafuata mapendekezo ya benchi la ufundi na mwalimu mzuri anafanya kazi na wachezaji wake kwa ushirikiano mkubwa.

  Previous articleVIDEO:DENIS NKANE ATOA SHUKRANI KWA KUFUNGA,MUDA UTAONGEA
  Next articleMZAMBIA HUYU AINGIA ANGA ZA SIMBA NA YANGA