MOSES Phiri, mshambuliaji wa Zanaco FC ya Zambia anatajwa kuzichonganisha timu kongwe Bongo, Simba na Yanga ambazo zote zinatajwa kuisaka saini yake.
Nyota huyo anatajwa kwamba amezungumza na mabosi wa Simba ambao wanahitaji huduma yake ila kabla hajamwaga wino na Yanga nao wanatajwa kubisha hodi.
Mambo yamebadilika kwa sasa na ushindani wa kuisaka saini yake unatajwa kuwa mkubwa na mpaka wakati huu habari zinasema kwamba hajasaini Yanga wala Simba.
Wakala wa Phiri ambaye anaitwa Nawa Nyambe amesema kuwa kuna ofa kutoka timu za Tanzania ambazo zinasaka saini yake.