HAJI MANARA: SIJUI LOLOTE KUHUSU OFISA HABARI WA SIMBA,NI NANI?

HAJI Manara Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa hajui jambo lolote kuhusu Ofisa Habari mpya wa Simba, Ahmed Ally.

Manara mwaka jana alisepa kwenye majukumu yake ndani ya Simba kutokana na mvutano uliokuwa ndani ya timu yake hiyo ya zamani ambayo aliwahi kusema kwamba anaipenda tangu akiwa mgogo.

Kwa sasa Manara anatimiza majukumu yake ndani ya kikosi cha Yanga ambacho kipo visiwani Zanzibar kwa ajili ya kushiriki Kombe la Mapinduzi na Yanga ni mabingwa watetezi.

Simba imemtangaza Ahmed Ally kwa sasa kuwa Ofisa Habari wa timu hiyo na ameshaanza kazi ya kuweza kutimiza majukumu yake muda mfupi baada ya kutambulishwa ndani ya Simba.

Alipoulizwa Manara na mwandishi wa Habari wa Global TV, kuhusu kujua juu ya Ofisa Habari mpya wa Simba, Manara alionekana akishangaa.

“Ofisa habari, ni nani kwani, mimi sijui na sikuwepo hapa naitwa Bugati,”.