Mwaka 2022 unaanza na habari njema kwa wateja wa DStv! Kuanzia tarehe 5 Januari 2022, DStv itaanza promosheni yake kabambe ijulikanayo kama ‘Panda Tukupandishe’ ambapo wateja wa DStv watapatiwa vifurushi vya juu ili kufurahia zaidi burudani katika kipindi hiki cha mwanzo wa mwaka.
Promosheni hii itadumu kwa miezi mitatu na ni kwa wateja wa vifurushi vya DStv Poa, Bomba, Shangwe na Compact.
Akitangaza promosheni hiyo, Mkuu wa cvm wa MultiChoice Tanzania Hilda Nakajumo, amesema kuwa katika promosheni hiyo, mteja wa DStv atakayelipia kifurushi cha juu ya kile anachotumia atapandishwa na kupewa kifurushi cha juu zaidi kwa mwezi mmoja bila gharama za ziada.
Mathalan, mteja wa DStv Poa (Sh 9,00) akilipia kifurushi cha juu yake ambacho ni DStv Bomba (Sh 21,000) atapandishwa na kupewa kifurushi cha DStv Shangwe (Sh 31,000) chenye chaneli zaidi ya 100
Hali kadhalika, mteja wa DStv Bomba atakayelipia kifurushi cha DStv Shangwe, atapandishwa na kupewa kifurushi cha DStv Compact chenye chaneli zaidi ya 130
Mteja wa kifurushi cha Shangwe, akilipia kifurushi cha Compact atapandishwa na kupatiwa kifurushi cha Compact Plus chenye chaneli zaidi ya 140 Huku mteja wa kifurushi cha Compact akilipia Compact Plus atapewa kifurushi cha juu kabisa cha DStv Premium chenye chaneli zaidi ya 150
“Tungependa kuona wateja wetu wakiendelea kupata burudani kipindi hiki cha mwanzo wa mwaka ambacho kinafahamika kwa kuwa na majukumu mengi. Promosheni hii inawawezesha wateja wetu kupata Habari, Burudani na elimu zaidi kwa kupata vifurushi vya juu vyenye chaneli nyingi zaidi. Tunaamini hii ni zawadi nzuri ya mwaka mpya kwa wateja wetu na tunaamini wataifurahia” alisema Hilda.
Mteja wa DStv Poa atakayelipia DStv Bomba na kupandishwa kwenda DStv Shangwe ataweza kufurahia Michuano ya AFCON 2022 ambayo itaanza kurindima January 9,2022. Pia atashuhudia michuano ya inayoendelea ya Spanish LALIGA na ligi ya Italian Serie A pia ataweza kufurahia tamthilia mbalimbali za ndani kama JUA KALI, KITIMTIM, DANGA na LA FAMILIA.
Mteja wa DStv Bomba atakayelipia DStv Shangwe na kupandishwa kwenda DStv Compact atapata uhundo kwa kushuhudia mechi za ligi kuu ya Uingereza EPL, michuano ya Carabao CUP, FA Cup, tamthilia mbalimbali na katuni kwaajili ya watoto.
Mteja wa DStv Shangwe atakayelipia DStv Compact atapandishwa kwenda DStv Compact Plus ambapo huko atafurahia michuano ya UEFA Champions League itakayoanza tarehe 15/2/2022 wakati Mteja wa DStv Compact atakayelipia DStv Compact Plus atapandishwa kwenda kifurushi cha juu zaidi cha DStv Premium ambapo huko atapata chaneli maarufu kama SuperSport Football Plus, ESPN 2 HP, SuperSport Cricket, SuperSport Golf, SuperSport Tennis HD, SuperSport Motorsport HD, SuperSport Rugby kushuhudia michezo mbalimbali kama michezo ya magari, tenis, NBA na Cricket.
Hilda amesema kuwa kunufaika na promosheni hii ni rahisi kwani mteja anachotakiwa kufanya ni kulipia kifurushi cha juu ya kile anachotumia na DStv itamzawadia kifurushi cha juu zaidi.
Bila shaka katika kipindi hiki cha miezi mitatu ya promosheni hii, wateja wa DStv watapata uhondo wa kuangalia chaneli nyingi zaidi na hivo kufurahia michezo mashindano mbalimbali ya kimataifa, tamthilia kali za ndani na nje, sinema, habari, vipindi maalum, Makala na bila kusahau vipindi motomoto vya Watoto. Kwa hakika itakuwa ni miezi mitatu ya burudani ya aina yake kwa wateja wa DStv.
Kwa maelezo zaidi kuhusu promosheni hii pamoja na vipindi motomoto vya DStv na huduma nyingine, tembelea www.dstvafrica.com. Ili kufurahia zaidi huduma za DStv, pakua App ya DStv ijulikanayo kama MyDStv App itakayokuwezesha kutazama vipindi vya DStv kwa kutumia simu yako, laptop au tablet popote ulipo.