Home Sports MTIBWA WAANZA KUIWINDA RUVU

MTIBWA WAANZA KUIWINDA RUVU

OFISA Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru, ameweka wazi juu ya maandalizi yao
kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting utakaochezwa
Januari 14, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mabati, Pwani.
 
Mtibwa Sugar ikiwa na kumbukizi nzuri ya kutoka kuichapa Costal Union 1-0, inashika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kucheza mechi 11 na kufanikiwa kupata pointi 10.
 
Akizungumza na Spoti Xtra, Kifaru alisema: “Maandalizi yetu yapo vizuri sana, tulianza tangu Jumatatu, tunafanya mazoezi kwa kuangalia wapi tulifanya kosa na kurekebisha na kuimarisha kikosi zaidi ili kupata ushindi. 
Previous articleDSTV YAFUNGUA MWAKA NA PANDA TUKUPANDISHE!
Next articleKOCHA SIMBA ASAINI KMC