Home Sports KOCHA SIMBA ASAINI KMC

KOCHA SIMBA ASAINI KMC

HITIMANA Thiery amesaini dili la mwaka mmoja kuinoa Klabu ya KMC inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kocha huyo hivi karibuni alisitisha mkataba wake na Klabu ya Simba ambayo inanolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco.

Alijiunga na Simba kwa ajili ya mashindano ya kimataifa kwa kuwa aliyekuwa kocha wa wakati huo Didier Gomes hakuwa na vigezo ambavyo vilikuwa vinatakiwa na Caf kwa wakati huo.

Hitimana amesema:”Nimesaini KMC hivyo ni baada ya kuweza kufikia makubaliano na yapo mengi yaliyopo ambayo yapo kwenye mkataba,”.

Previous articleMTIBWA WAANZA KUIWINDA RUVU
Next articleSIMBA QUEENS WAIPIGA BITI YANGA PRINCES