
MAJEMBE MAPYA YANGA KUANZA KAZI
RASMI uongozi wa Yanga umefunguka kuwa kuna uwezekano mkubwa wa wachezaji wapya watakaosajiliwa na timu hiyo katika dirisha hili dogo la usajili kutumika katika michuano ya Kombe la Mapinduzi itayoanza kutimua vumbi Januari visiwani Zanzibar. Yanga katika dirisha hili dogo la usajili wanahusishwa kwa karibu na baadhi ya wachezaji akiwemo mshambuliaji Jean Marc Makusu anayekipiga DC Motema Pembe na kiungo mshambuliaji Fabrice Ngoma anayekipiga Raja Casablanca ya Morroco. Pia…