Home Sports PABLO APEWA JUKUMU HILI SIMBA

PABLO APEWA JUKUMU HILI SIMBA

IKIWA kwa sasa harakati za usajili wa dirisha dogo limeanza,mabosi wa Simba wameamua kumuachia jukumu la kupendekeza  Kocha Mkuu wa Simba Pablo Franco wa kuweza kupendekeza maeneo anayohitaji waweze kuyaboresha.

Taarifa kutoka benchi la ufundi wa Simba zimeeleza kuwa kwa sasa hakuna mapendekezo ambayo yametolewa lakini viongozi wanasubiri taarifa kutoka kwa Pablo ili waweze kufanya usajili.

“Bado hakuna usajili ambao tumeweza kufanya kwa sasa lakini suala hilo lipo na Pablo anasubiriwa kutoa mapendekezo ya wachezaji ambao wanahitajika hivyo ni suala la kusubiri,” ilieleza taarifa hiyo.

Nafasi ambazo zinapewa chapuo ya kuweza kuongezewa nguvu ndani ya Simba ni eneo la kiungo mshambuliaji na mchezaji,beki wa kati pamoja mshambuliaji mmoja.

Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu, amesema kuwa suala la usajili linategemea ripoti ya benchi la ufundi.

“Kuhusu usajili inategemea benchi la ufundi linasema nini lakini niwatoe hofu mashabiki kikosi chetu ni imara na wachezaji wanapambana muda wote kutimiza majukumu,” amesema .

 

Previous articleMABAO SABA KUIKOSA TANZANIA PRISON LEO
Next articleKIKOSI CHA YANGA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA TANZANIA PRISONS