
BEKI WA MABINGWA ATUA SINGIDA BIG STARS
BEKI wa Yanga ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho msimu wa 2021/22 ametua ndani ya kikosi cha Singida Big Stars. Yanga jana Julai 2 iliweza kukamilisha msimu kwa kutwaa Kombe la Shirikisho kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Coastal Union kwa ushindi wa penalti 4-1 baada ya dk 120 kukamilika…