Home Sports JONAS MKUDE NI MKALI WAO SIMBA,ANASTAHILI PONGEZI KIDOGO

JONAS MKUDE NI MKALI WAO SIMBA,ANASTAHILI PONGEZI KIDOGO

KWENYE tamasha la leo la Simba Day ambalo linatarajiwa kufanyika Uwanja wa Mkapa kwa mastaa wa Simba kuna Legend mmoja anaitwa Jonas Mkude.

Kiungo huyo anastahili heshima kutokana na kudumu ndani ya kikosi hicho kwa muda mrefu akiwa ni mchezaji pekee ambaye amedumu hapo tangu alipopandisha msimu wa 2011/12 kutoka Simba B.

Mastaa wengine wote ambao alipandishwa nao wamekwama kufurukuta ndani ya Simba ikiwa ni pamoja na Said Ndemla ambaye kwa sasa yupo Singida Big Stars,Ibrahim Ajibu ambaye yupo zake ndani ya Azam FC pia Edward Christopher,Abdallah Seseme yupo zake Kagera Sugar,Miraj Athuman,’Sheva’.

Kwa nyota wote ambao alipandishwa nao hakuna ambaye atakuwepo kwenye tamasha hilo zaidi ya Kocha Msaidizi Seleman Matola ambaye zama wakipanda alikuwa ni kocha ndani ya Simba.

Mkude anastahili heshima licha ya kuwa na kesi za mara kwa za utovu wa nidhamu jambo ambalo liliwahi kupekelea kuweza kupelekwa hopitali kwa ajili ya vipimo zaidi.

Mshikaji wake Chris Mugalu hatakuwa kwenye kikosi cha leo kwa kuwa mkataba wake umeshavunjwa na mabosi kwa makubaliano maalumu huku Bernard Morrison yeye akiwa ndani ya Yanga.

Previous articlePITSO:YANGA INAHITAJI MUDA KUWA IMARA
Next articleHAJI MANARA NA INJINIA WAITWA KWENYE KAMATI YA MAADILI