Home Sports PITSO:YANGA INAHITAJI MUDA KUWA IMARA

PITSO:YANGA INAHITAJI MUDA KUWA IMARA

KOCHA mwenye uzoefu mkubwa Afrika raia wa Afrika Kusini ambaye aliweza kubwaga manyanga ndani ya Klabu ya Al Ahly ya Misri,Pitso Mosimane amesema kuwa Klabu ya Yanga ina wachezaji bora lakini wanahitaji muda kuwa imara.

Pitso alikuwepo kwenye Tamasha la Wiki ya Mwananchi,Agosti 6,2022 alishuhudia Uwanja wa Mkapa ubao ukisoma Yanga 0-2 Vipers kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa.

Jana alikwea pipa kurejea nchini Afrika Kusini baada ya ziara yake Bongo kufika ukomo kwa kuwa alialikwa na Yanga kwa ajili ya kuwa kwenye tamasha hilo.

“Nimewaona wachezaji bora lakini wanahitaji muda kidogo ili waweze kuandaliwa na kuwa na makali zaidi.

“Licha ya kuwa na kipaji na uwezo lakini wachezaji walikuwa wanacheza kawaida sana ni sahihi nikisema kuwa walikuwa wanasherehekea pamoja na mashabiki,” amesema.

Tamasha la Yanga lilianza rasmi mwaka 2009 na limekuwa likizidi kujipatia umaarufu Tanzania na nje ya Tanzania.

Mabao ya Vipers ambao walipachika mabao hayo kila kipindi bao moja yalijazwa kimiani na Milton Karisa dk ya 01 na Bright Anukani ambaye pigo lake la kona lilijaa mazima wavuni na kumshinda Djigui Diarra ilikuwa dk ya 63.

Previous articleGEITA GOLD WASHUSHA MTU MWINGINE WA KAZI
Next articleJONAS MKUDE NI MKALI WAO SIMBA,ANASTAHILI PONGEZI KIDOGO