Home Sports GEITA GOLD WASHUSHA MTU MWINGINE WA KAZI

GEITA GOLD WASHUSHA MTU MWINGINE WA KAZI

 WACHIMBA madini,Geita Gold hawatanii kwa kuwa wana jambo lao na leo Agosti 7,2022 wameweza kumtambulisha nyota mpya katika kikosi hicho.

Timu hiyo inakwenda kushiriki mashindano ya kimataifa Afrika baada ya kumaliza ligi ikiwa nafasi ya nne hivyo inajipanga kuwa ya kipekee.

Ni beki Yahya Mbegu leo ametambulishwa kuwa mchimba madini mapya baada ya Agosti 4 kutambulishwa kwa Miraj Athuman ambaye alikuwa anacheza KMC.

Kupitia ukurasa wao wa kijamii rasmi wa Geita Gold wameandika namna hii:”Geita Gold FC tunayofuraha kuwataarifu kuwa tumefikia makubaliano na mlinzi wa kushoto Yahya Mbegu kutumikia klabu yetu kwa mkataba wa miaka miwili ( 2).

“Mbegu amejiunga na wachimba madini akitokea Polisi Tanzania. Sasa Mbegu imetunzwa na mashimo ya dhahabu,”.

Previous articleMSERBIA MPYA WA SIMBA AMEANZA KAZI BAADA YA KUTAMBULISHWA
Next articlePITSO:YANGA INAHITAJI MUDA KUWA IMARA