Home International MSERBIA MPYA WA SIMBA AMEANZA KAZI BAADA YA KUTAMBULISHWA

MSERBIA MPYA WA SIMBA AMEANZA KAZI BAADA YA KUTAMBULISHWA

MSERBIA wa Simba muda mfupi baada ya kutambulishwa leo alikuwa miongoni mwa wachezaji ambao wamefanya mazoezi ya mwisho Uwanja wa Mkapa.

Nyota huyo ametambulishwa leo Agosti 7,2022 ni Dejan Georgijević ambaye ni mshambuliaji akitokea Klabu ya Domzale.

Usajili huo wa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu,Zoran Maki ni maalumu kwa ajili ya kuboresha kikosi kwa msimu wa 2022/23.

Kesho Agosti 8/2022 anatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji ambao watakuwepo kwenye kilele cha Tamasha la Simba Day.

Simba itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya St George kutoka nchini Ethiopia.

Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa bado hawajafunga usajili watatambulisha wachezaji wapya wakifika makubaliano mazuri.

 

Previous articleSINGIDA BIG STARS INAFIKIRIA KIMATAIFA
Next articleGEITA GOLD WASHUSHA MTU MWINGINE WA KAZI