Home Sports SINGIDA BIG STARS INAFIKIRIA KIMATAIFA

SINGIDA BIG STARS INAFIKIRIA KIMATAIFA

UONGOZI wa Singida Big Stars,umeweka wazi kwamba malengo yao ni kumaliza katika nne za juu ili waweze kushiriki mashindano ya kimataifa.

Timu hiyo ambayo inatumia Uwanja wa Liti kwa mechi za nyumbani ina maingizo mapya ya kimataifa ikiwa ni pamoja na Meddie Kagere na Pascal Wawa ambao waliwahi kucheza Simba.

 Ofisa Habari wa Singida ig Stars,Hussein Massanza alisema kuwa wanaamini kwamba ushindani utakuwa mkubwa nao wanafikiria kufanya kazi kubwa.

“Kumaliza kwenye nafasi nne za juu ni malengo yetu ambayo yatatupa nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa ipo wazi na tutapambana kufanya vizuri.

“Usajili wetu umezingatia mapendekezo ya benchi la ufundi,tupo tayari kwa ajili ya ushindani na wachezaji ambao tupo nao wapo vizuri pia” amesema Massanza.

Timu hiyo imesajili wachezaji wakitaifa na kimataifa ikiwa ni pamoja na Said Ndemla,Pascal Wawa,Meddie Kagere.

Previous articleTIMU YA TAIFA BEACH SOCCER KAZINI LEO
Next articleMSERBIA MPYA WA SIMBA AMEANZA KAZI BAADA YA KUTAMBULISHWA