Home Sports TIMU YA TAIFA BEACH SOCCER KAZINI LEO

TIMU YA TAIFA BEACH SOCCER KAZINI LEO

LEO kikosi cha Timu ya Taifa ya Soka la Ufukweni ‘Beach Soccer’ kitakuwa na mchezo wa marudiano wa kufuzu AFCON (BSAFCON) dhidi ya Malawi kwa ajili ya kufunga hesabu yake ya maandalizi hayo kwenye Fukwe za Coco jijini Dar es Salaam.

Katika mazoezi ya mwishomwisho yaliyofanyika Ijumaa na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa michezo wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wilfred Kidau, yalionekana kuwa na hamasa kubwa.

Kocha wa kikosi hicho, Boniface Pawassa kwa kushirikiana na Kocha wa Mkuu wa Timu ya Taifa ya Oman, Talib Hilal, walionekana wakifundisha zaidi mbinu za ufungaji jambo linaloashiria wawili hao kuhitaji ushindi mnono mbele ya Malawi.

Kwenye mchezo wa kwanza wa kufuzu katika michuano hiyo, uliopigwa nchini Malawi, timu hiyo ilipoteza dhidi ya Malawi kwa kufungwa mabao 3-2, jambo ambalo limewafanya kuongeza juhudi za mazoezi ili waweze kupata ushindi mnono nyumbani na kujitengenezea nafasi ya kuendelea katika hatua inayofuata ya mashindano hayo.

Pawasa amesema wapo tayari kwa ajili ya ushindani na wanaamini kwamba watafanya vizuri.

Previous articleUZI MPYA WA SIMBA WAZINDULIWA
Next articleSINGIDA BIG STARS INAFIKIRIA KIMATAIFA