Home Sports HAJI MANARA NA INJINIA WAITWA KWENYE KAMATI YA MAADILI

HAJI MANARA NA INJINIA WAITWA KWENYE KAMATI YA MAADILI

KITENDO cha kuibuka Uwanja wa Mkapa,Agosti 6,2022 na kuwatambulisha wachezaji, Haji Manara aliyekuwa msemaji wa Yanga akiwa kifungoni kimemrejesha kwa mara nyingine Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF).

Ikumbukwa kwamba Manara alifungiwa miaka miwili na hakupaswa kushughulika na masuala ya mpira kwa muda huo.

 Pia Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said naye ni miongoni mwa walioitwa kwenye kamati hiyo kwa kuwa alipewa taarifa kuhakikisha kuwa Yanga inaheshimu maamuzi ya kamati.

TFF kupitia Sekretarieti yake imemfungulia mashtaka ya kimaadalili Rais wa Yanga na Manara kutokana na kitendo cha Manara kuweza kujishughulisha na masuala ya mpira.

Sababu ya Manara kufungiwa ni kile kilichoelezwa na kamati kuwa aliweza kugombana hadharani na Rais wa TFF,Wallace Karia kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho wa fainali kati ya Yanga na Coastal Union uliochezwa Arusha.

Manara Agosti 6,2022 alihudhuria tamasha la Wiki ya Mwananchi na kuwatambulisha wachezaji huku akidai kwamba amealikwa akiwa ni msherehesaji tu alipomaliza tukio la kuwatambulisha wachezaji alisepa jumlajumla.

Taarifa imeeleza kuwa tayari wameshapelekewa barua walalamikiwa akiwemo Haji Manara na kamati itapanga tarehe ya kusikiliza mashitaka hayo.

Previous articleJONAS MKUDE NI MKALI WAO SIMBA,ANASTAHILI PONGEZI KIDOGO
Next articleSIMBA WATAMBA,NABI ASHUSHA PRESHA AITANGAZIA KIAMA SIMBA