Home Sports FT:SIMBA 2-0 ST GEORGE,UWANJA WA MKAPA

FT:SIMBA 2-0 ST GEORGE,UWANJA WA MKAPA

SIMBA imeshinda mabao 2-0 dhidi ya St George kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Ni mchezo maalumu kwenye kilele cha Wiki ya Simba ikiwa ni mchezo wa kwanza kwa Zoran Maki ambaye ni raia wa Serbia.

Mabao ya Simba yamefungwa na mzawa Kibu Dennis na Nelson Okwa ambaye aliingia kipindi cha pili akitokea benchi.

Maki amesema kuwa wamefurahi kupata ushindi kwenye mchezo wa kirafiki na wanakwenda kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga unaoatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa,Agosti 13.

“Tunajua kwamba mchezo ulikuwa mzuri na wachezaji wameweza kufanya kikubwa bado kuna kazi ya kuweza kufanya ili kuweza kuongeza kitu kwenye kikosi chetu,”.

 

Previous articleMAPUMZIKO:SIMBA 1-0 ST GEORGE
Next articleKWENYE JUMUIYA YA MADOLA TANZANIA IMEPATA MEDALI