MAANDALIZI MUHIMU KWA SERENGETI GIRLS

    KUWEZA kufuzu Kombe la Dunia ni hatua moja muhimu na kuweza kufanya maandalizi mazurini hatua ambayo inahitajika kuweza kufanyika kwa sasa.

    Tunaona kwamba Serengeti Girls ambayo ni Timu ya Taifa ya Wasichana chini ya miaka 17 ina kibarua cha kufanya kimataifa.

    Kombe la Dunia lipo njiani ambapo inatarajiwa kuweza kufanyika nchini India kuanzia Oktoba 11-30 mwaka huu.

    Mipango mikubwa ifanyike kwa umakini kuanzia sasa kwa kuwa ili uweze kushinda ni muhimu kufanya maandalizi kwani kila kitu kinawezekana.

    Hatua ya makundi ni moja ya kazi kubwa na ngumu kwa kuwa hapa kila timu ambayo imeweza kufika ni bora na inahitaji matokeo chanya katika mechi ambazo itacheza.

    Ikumbukwe kwamba tiketi ya kuweza kuwa hapa ambapo mmefika kwa sasa haikupatikana kwa wepesi bali kujitoa na kucheza bila kuchoka kwenye mechi zote za ushindani.

    Ule ushindi wa jumla ya mabao 5-1 mbele ya Cameroon ilikuwa ni mpango kazi mkubwa na kila mmoja aliweza kuona namna kazi ilivyokuwa ngumu katika kusaka ushindi.

    Hilo halikuwa jambo jepesi kwani ilionekana jasho la wachezaji lilimwagika huku mbinu za benchi la ufundi nazo zikitumika kwenye kusaka ushindi wa mechi hizo ngumu.

     U 17 wapo kundi D wameshawatambua wapinzani wao ambao wanakwenda kupambana nao hilo ni jambo lingine la kuweza kuanza kujipanga kupata ushindi.

    Kila kitu kinawezekana hasa kwa kufanya maandalizi mazuri kabla ya kuingia kwenye uwanja wa mapambano na tunaamini kwamba mipango imeshaanza.

    Uzuri ni kwamba U 17 wameonja ile ladha ya kuweza kuwa kwenye mechi kubwa na za kimataifa sasa wanakwenda kuanza kucheza mechi kubwa katika hatua kubwa zaidi.

    Historia itawakumbuka daima na mtakuwa kwenye kumbukumbu ya wale ambao wataimbwa miaka yote kwa kuweza kupiga hatua hiyo kubwa.

    Yote kwa yote ni muhimu kuelewa kwamba kwa namna yoyote ile mafanikio kwenye hatua inayofuata bado yapo kwenye miguu yenu U 17.

    Kutoka kwa ukanda wa Afrika Mashariki Tanzania itakuwa inapepersuha Bendera na inakutana na timu kutoka  Japan,Canada na Ufaransa.

    Timu hizi ni kubwa na zote zinaonekana namna ambavyo zinawachezaji wakubwa lakini haina maana ya kuweza kuwahofia kisa majina yao ni makubwa.

    Haijalishi ni timu kubwa kwa namna gani kwa upande wa uchumi pamoja na uwekezaji bado kuna nafasi ya kuweza kupata matokeo kwenye mechi ambazo zinatuhusu.

    Kikubwa ni kuwa na nidhamu kwenye mechi ambazo mtacheza na hilo ni jambo la msingi kuzingatiwa kwa kila mchezaji.

    Kambi ambayo imewekwa kwa sasa ikawe na manufaa kwa wachezaji pamoja na benchi la ufundi kuweza kujua namna ya kwenda kimataifa kupeperusha bendera ya Tanzania.

    Kwa walipoweza kufika wanapaswa kuongeza juhudi zaidi kuweza kupeperusha bendera ya Tanzania na Afrika kiujumla katika upande wa soka la Wanawake.

    Ukweli ni kwamba kila timu ambayo imeweza kupenya hapa ni kubwa na ni imara hivyo maandalizi na yaanze sasa kwa ajili ya kwenda kufanya kazi nzuri huko India.

    Kwenye ulimwengu wa mpira kauli yetu ni kwamba kila kitu kinawekana kwa mipango sahihi na kufanya kile ambacho kitakuwa na matokeo mazuri pale watakapokuwa kwenye uwanja wa mchezo husika.

    Kazi ya mashabiki ni kuendelea kufanya dua kwa wachezaji pamoja na benchi la ufundi ili waweze kupata matokeo mazuri.

    Oktoba ipo njiani kinachotakiwa ni kufanya maandalizi mazuri ili kuweza kutusua katika mashindano haya makubwa na yenye hadhi za kimataifa.

    ReplyForward

    Previous articleSIMBA WATAMBA,NABI ASHUSHA PRESHA AITANGAZIA KIAMA SIMBA
    Next articleMERIDIANBET WAWATEMBELEA BODA BODA, WAWAPA UJUMBE USALAMA NI MUHIMU