FT: Mashujaa FC 0-3 Simba SC NBC Premier League

FT: Mashujaa FC 0-3 Simba SC ni matokeo ya mchezo wa NBC Premier League uliochezwa leo Mei 14, 2026 Uwanja wa Lake Tanganyika, mwisho wa reli Kigoma.

Magoli ya Simba SC yamefungwa na Clatous Chama dakika ya 5 na dakika ya 70 huku kamba ya tatu ikifungwa na Seleman Mwalimu dakika ya 90+2.

Matokeo haya yanamfanya mnyama kufikisha jumla ya poli 52 akiwa nafasi ya pili kwenye msimamo tofauti ya pointi mbili na kinara Yanga SC mwenye pointi 54 wote wamecheza mechi 23.

Huu ni mchezo wa mzunguko wa pili, mnyama akishinda nje ndani dhidi ya wapinzani wao Mashujaa FC ukiwa ni mchezo wa kwanza kupoteza kwa wenyeji wakiwa nyumbani.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.