
VIDEO: CHEKI TIZI LA WAPINZANI WA SIMBA, de AGOSTO
WAPINZANI wa Simba kimataifa de Agosto kutoka Angola leo Oktoba 15,2022 wamefanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa kesho Oktoba 16,2022 Uwanja wa Mkapa
WAPINZANI wa Simba kimataifa de Agosto kutoka Angola leo Oktoba 15,2022 wamefanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa kesho Oktoba 16,2022 Uwanja wa Mkapa
ALLY Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kesho Oktoba 16,2022 baada ya ule wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao kusoma Yanga 1-1 Al Hilal. Alfajiri ya leo Oktoba 15,2022 kikosi cha Yanga kinachonolewa…
JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amemshutumu Kocha Mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta kwa kumpa presha mwamuzi wa mchezo huo Michael Oliver. Jumapili Arsenal ilifanikiwa kushinda mabao 3-2 dhidi ya Liverpool kwenye mchezo wa Ligi Kuu England Uwanja wa Emirates. Penalti ya staa Bukayo Saka ambayo ilizua utata na ilileta bao la tatu kwa Arsenal…
WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Azam FC baada ya kete yao ya kwanza kupoteza ugenini wanatarajiwa kurejea leo kuanza kujipanga upya. Juzi Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Mfaransa Denis Lavagne ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Martrys of February ukisoma Al Akhadar 3-0 Azam FC nchini Libya. Azam FC ina kibarua cha kusaka…
MSAFARA wa wachezaji wa Simba pamoja na benchi la ufundi umewasili salama nchini Angola leo Oktoba 8,2022 kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya de Agosto. Ni jumla ya wachezaji 24 ambao walikuwa kwenye msafara huo miongoni mwao ni pamoja na Aishi Manula, Ally Salim na…
TIMU ya Taifa ya Watu wenye ulemavu Tanzania (Tembo Warriors,) imefuzu kuingia katika hatua 16 bora katika mashindano ya kombe la dunia la mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu. Tanzania ilipata ushindi wake wa kwanza wakiifunga Uzbekistan mabao 2-0 huko Uturuki yanapoanyika mashindano hayo. Tembo Warriors sasa watakutana na Japan katika mchezo unaotarajiwa kuchezwa…
MABAO 6 yalikusanywa kwenye mechi tatu za Ligi Kuu Bara zilizochezwa Oktoba 4,2022 katika msimu wa 2022/23. Mchezo uliokusanya mabao mengi ulikuwa ni ule Ruvu Shooting 1-2 Yanga ikiwa ni mabao matatu kwenye mchezo mmoja. Watupiaji kwenye mchezo huo ni Feisal Salim dakika ya 52 na Bakari Mwamnyeto dakika ya 71 lile la Ruvu Shooting…
CEDRICK Kaze, Kocha Msaidizi wa Yanga ameweka wazi kuwa kweye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika hawadharau wapinzani wao na badala yake wanahitaji ushindi dakika za mwanzo. Yanga chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi inakibarua cha kusaka ushindi Ligi ya Mabingwa raundi ya Pili dhidi ya Al Hilal mchezo unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 8, Uwanja wa…
NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi zao zote za kitaifa na kimataifa kutokana na uwepo wa wachezaji wenye uwezo. Mchezo ujao Yanga unatarajiwa kuchezwa Oktoba 3,2022 utakuwa wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting na kete yao inayofuata kimataifa itakuwa dhidi ya Al Hilal, Uwanja wa Mkapa,…
MIPANGO ya ushindi kusukwa inaanza kwa wachezaji wale waliopo ndani ya uwanja na wale wanaokaa benchi kusoma mchezo unavyoendelea. Ndani ya ligi msimu wa 2022/23 wapo mastaa ambao wamekuwa wakali wakianzia benchi kwa kuwa walipoingia walifanikiwa kubadilisha namba kwenye ubao. Hapa tunakuletea baadhi ya nyota ambao wamekuwa na makali wakianzia benchi namna hii:- Feisal Salum…
UONGOZI wa Yanga leo Septemba 27,2022 umemtangaza Adre Mtine kutoka Zambia kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu mpya wa klabu hiyo. Ni mkataba wa miaka miwili CEO huyo amepewa kufanya kazi ndani ya Yanga ambapo utambulisho wake umefanywa na Rais wa Yanga, Injinia Hers Said. Anakuja kuchukua mikoba ya Senzo Mbatha raia wa Afrika Kusini ambaye mkataba…
MWANDISHI Mkongwe kwenye masuala ya mpira Bongo, Saleh Ally ‘Jembe’ amesema kuwa winga wa Klabu ya Yanga Bernard Morrison anatakiwa kurekebisha tabia yake ya kushindwa kujizuia hasira zake na mwishowe kufanya matukio ambayo yanampa hasara. Nyota huyo kutokana na makosa hayo amesababisha afungiwe kucheza michezo mitatu ya Ligi Kuu ya NBC pamoja na faini ya…
MSHAMBULIAJI wa Tottenham, Harry Kane raia wa England ameweka wazi kuwa kasi ambayo ameanza nayo mshambuliaji mpya ndani ya Manchester City, Erling Haaland ni nzuri ila naye ataongeza juhudi kutimiza majukumu yake. Haaland raia wa Norway amekuwa chachu ya matokeo mazuri uwanjani ametupia jumla ya mabao 14 kwenye mechi za mashindano yote. Ni namba moja…
MVURUGANO ambao huwa unapatikana baada ya matokeo yasiyotarajiwa kwa wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania kwenye benchi la ufundi pamoja na wachezaji huwa unakuwa sio wa kawaida. Hii inatokea kwa sababu kila mmoja anapoingia uwanjani mpango wake ni kuona timu inapata matokeo na pale inaposhindikana. Uzuri ni kwamba mchezo wa mpira ni mchezo wa…
WAZAWA wawili ambao kwa sasa wanakinoa kikosi cha Simba wote wameanza mwendo wao kwa kasi nzuri wanastahili pongezi na kuongza juhudi zaidi katika kutimiza majukumu yao. Kocha Mkuu, Juma Mgunda ameanza kibarua kwenye nyakati ngumu kwa kuwa timu ilikuwa bado haijaungana na muunganiko wake ulikuwa unatafutwa. Kuondoka kwa Zoran Maki na mikoba yake kuwa mikononi…
MWANDISHI mkongwe katika masuala ya michezo Afrika Mashariki na kati ameweka wazi kuwa mchezo wa Ligi ya Mabingwa kati ya Zalan FC na Yanga umekwisha, Yanga walipata bahati kwa kuwa hawakupata timu ngumu kimataifa hilo limewasaidia kujipanga kuwa vizuri na hata Simba ingewapata hao ingepata bahati. Kuhusu de Agosto ya Angola ambao ni wapinzani wa…
ANAZIDI kuimarika akiwa langoni, Aboutwalib Mshery na alipewa dakika 90 mbele ya Zalan FC mchezo wa kwanza na ule wa pili alitumia dakika 45. Sababu ya kupewa nafasi kikosi cha kwanza ni kutokana na maumivu ambayo alikuwa nayo kipa namba moja, Diarra Djigui hivyo kazi ikawa kwake kutimiza majukumu ya timu. Kutinga hatua ya awali…