Home Uncategorized MTAMBO WA MABAO SIMBA WAFICHUA SIRI YA KUTUSUA

MTAMBO WA MABAO SIMBA WAFICHUA SIRI YA KUTUSUA

MKALI wa kucheka na nyavu ndani ya kikosi cha Simba, Moses Phiri amesema kuwa kikubwa ambacho kinampa nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi anazocheza ni ushirikiano na wachezaji wote wa timu hiyo.

Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika katupia mabao matano na kwenye Ligi Kuu Bara katupia mabao matano na kumfanya awe ametupia mabao 10 msimu wa 2022/23 akiwa na uzi wa Simba.

 Phiri raia wa Zambia ni miongoni mwa mastaa ambao wametimiza majukumu yao vema na hatimaye timu hiyo imetinga hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Nyota huyo pia ana pasi moja ya bao ambayo alitoa kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Mkapa wakati timu hiyo iliposhinda mabao 5-0 na yeye alitupia bao moja wakati wakisepa na pointi tatu mazima.

“Kila mmoja anapenda kuona tunapata matokeo na hilo lipo kwa wachezaji wote ambao tunavaa jezi ya Simba tukiwa kwenye majukumu yetu uwanjani.

“Kinachofanya niweze kufunga ama kutoa pasi ya bao ni ushirikiano ambao upo kwa wachezaji wote kwani kila mmoja anafanya kazi ile ambayo anapewa kuifanya hivyo bado tunaendelea kupambana.

“Mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi ili kutushangilia kwa kuwa uwepo wao unatuongezea nguvu ya kuendelea kupambana zaidi,” amesema.

Previous articleMAYELE: BADO TUNA NAFASI KIMATAIFA
Next articleKIPA KEPA KUIKOSA ARSENAL JUMAPILI