Home Sports MAYELE: BADO TUNA NAFASI KIMATAIFA

MAYELE: BADO TUNA NAFASI KIMATAIFA

NYOTA wa Yanga, Fiston Mayele amesema kuwa bado wana nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi za kimataifa kwa kuwa morali bado ipo.

Nyota huyo ambaye kwenye mechi dhidi ya Zalan FC alifunga jumla ya hat trick mbili, mchezo wa kwanza na ule wa pili ni namba moja kwa utupiaji ndani ya Yanga.

Alianza kikosi cha kwanza wakati ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Yanga 0-0 Club Africain mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho.

Kibarua kinachofuata ni ugenini, mchezo unatarajiwa kuchezwa Novemba 9,2022 nchini Tunisia.

Mayele amesema:”Ilikuwa ni kazi kubwa kwetu kutafuta matokeo ila bahati mbaya tukashindwa kupata ushindi licha ya kupata nafasi.

“Nina amini benchi la ufundi limeona yote ambayo tumekosea na watafanyia kazi ili wakati ujao tupate matokeo mazuri kwani muda bado upo.

“Mashabiki wasikate tamaa wazidi kutuombea ili tupate matokeo kwenye mechi za kimataifa ushindni ni mkubwa na kila timu inahitaji matokeo,”

Previous articleDILUNGA AFICHUA KUHUSU SIMBA
Next articleMTAMBO WA MABAO SIMBA WAFICHUA SIRI YA KUTUSUA