Simba SC 2-1 Pamba Jiji FC, Gueye Man of The Match

Simba SC 2-1 Pamba Jiji FC, Gueye Man of The Match ni baada yakuvuna pointi 3 muhimu katika mchezo wa NBC Premier League, Uwanja wa KMC Complex, Juni 14, 2026.

Magoli ya Simba SC yalifungwa na Ellie Mpanzu dakika ya 7 na Libase Gueye dakika ya 64 katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Goli pekee la Pamba Jiji FC lilifungwa na Mathew Tegisi dakika ya 18 ya mchezo huo. Huu ni mzunguko wa pili wababe hawa wanakutana.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza ubao wa Kirumba, Mwanza ulisoma Pamba Jiji FC 1-1 Simba SC, waligawana pointi mojamoja, Juni 14, 2026 pointi zote ni mali ya mnyama.

Ushindi huo unaifanya Simba SC kufikisha jumla ya pointi 61 kwenye msimamo nafasi ya 2 kinara ni Yanga SC mwenye pointi 63 wote wamecheza jumla ya mechi 26.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.