MCHEZO wa NBC Premier League uliochezwa leo Juni 16, 2026 Uwanja wa Majaliwa hakuna timu ambayo imepata bahati yakufunga goli ndani ya dakika 90.
Ubao wa Uwanja wa Majaliwa umesoma Namungo FC 0-0 TRA United, moja ya mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa uwanjani.
Wababe hawa wawili wamegawana pointi mojamoja katika ligi namba 6 kwa ubora Afrika kugota mwisho.
Namungo FC wanafikisha pointi 27 nafasi ya 12 na TRA United pointi 41 nafasi ya 5 zote zikiwa zimecheza mechi 27 zimesaliwa na mechi 3 kukamilisha mzunguko wa pili 2025/26.