Azam FC 2-0 Mashujaa FC

Azam FC wameibuka na ushindi kwenye mchezo wa mzunguko wa pili dhidi ya Mashujaa FC kwenye mchezo wa NBC Premier League uliochezwa leo Juni 16, 2026 Uwanja wa Azam Complex.

Baada ya dakika 90 ubao umesoma Azam FC 2-0 Mashujaa FC, magoli yakifungwa na Sadio Kanoute dakika ya 39 na James Akaminko dakika ya 41.

Akaminko amechaguliwa kuwa nyota wa mchezo. Matokeo hayo yanaifanya Azam FC kufikisha pointi 58 nafasi ya 3, Mashujaa FC pointi 27 nafasi ya 11.

Mashujaa FC wamepoteza mchezo wa pili mfululizo ndani ya Juni 2026 baada yakupoteza mchezo uliopita dhidi ya Yanga SC kwa kufungwa magoli 2-0.

Hivyo ndani ya dakika 180 wameruhusu kufungwa magoli 4 nakupoteza pointi 6 mazima ndani ya ligi namba 6 kwa ubora Afrika.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.