Home Uncategorized NABI ABAINISHA UGUMU ULIOPO

NABI ABAINISHA UGUMU ULIOPO

KUELEKEA kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC, Nasreddine Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa wapo tayari kuwakabili wapinzani wao.

Kocha huyo amebainisha kuwa ratiba ni ngumu ndani ya ligi hivyo wanapambana nayo kwa ajili ya kupata matokeo.

Nabi anaingia uwanjani akiwa na kumbukumbu ya kukusanya pointi moja mbele ya Simba kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Sare ya kufungana bao 1-1 ilisomeka baada ya dakika 90 kesho anawakabili KMC ambao wametoka kushinda mabao 2-1 dhidi ya Azam FC.

Nabi amesema:”Mchezo wetu dhidi ya KMC utakuwa na ushindani mkubwa hilo tunalitambua na kila mchezaji yupo tayari kwa ajili ya kuona timu inapata matokeo.

“Tunafahamu kuwa ratiba yetu ni ngumu, tunafanya kila jitihada kuendana na uhalisia unaotukabili kwa sasa. Tuna mechi ngumu mbele yetu na huo ndio ukweli ambao tunapaswa kupambana nao. Sio suala la nani atacheza ni suala la alama tatu,” amesema.

Previous articleKMC WAIVUTIA KASI YANGA
Next articleVIDEO:KMC: TUNAKWENDA KUCHEZA NA TIMU BORA,TUNATAKA POINTI TATU ZA YANGA