Home Sports KMC WAIVUTIA KASI YANGA

KMC WAIVUTIA KASI YANGA

 BAADA ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Azam FC kituo kinachofuata kwa KMC ni dhidi ya Yanga mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa,Oktoba 26.

Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na wanaamini kwamba watapata matokeo.

Kwenye msimamo KMC ipo nafasi ya tatu inakutana na Yanga ikiwa nafasi ya pili ndani ya ligi na vinara ni Simba.

“Kila kitu kinakwenda sawa na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Yanga na tunaamini kwamba tutapata matokeo.

“Kikubwa ni kuona kwamba kila mmoja anahitaji kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wetu Yanga tunawaheshimu nao wanatutambua kwamba tunaweza,” amesema.

Previous articleSIMBA KUPATA ADHABU KISA MECHI YA YANGA
Next articleNABI ABAINISHA UGUMU ULIOPO