Simba na Azam Kukutana Fainali ya CRDB Federation Cup Pemba

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza kuwa mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB Bank (CRDB Federation Cup) kati ya Simba SC na Azam FC utafanyika Julai 4, 2026 saa 11:00 jioni.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF, fainali hiyo itachezwa katika Gombani Stadium, ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha rasmi mashindano yote ya TFF kwa msimu wa 2025/2026.

Simba SC ilitinga hatua ya fainali baada ya kuiondoa Coastal Union FC katika mchezo wa nusu fainali, huku Azam FC ikifuzu baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya Young Africans SC (Yanga SC), ambao walikuwa mabingwa watetezi wa mashindano hayo.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa wa ushindani mkubwa kutokana na ubora wa timu zote mbili, huku kila upande ukisaka kumaliza msimu kwa kutwaa taji hilo muhimu na kujihakikishia nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa msimu ujao.

Ratiba ya Fainali

📅 Julai 4, 2026
Saa 11:00 Jioni
Simba SC vs Azam FC
🏟️ Gombani Stadium