Home Uncategorized YANGA KUSEPA KUWAFUATAA WAARABU

YANGA KUSEPA KUWAFUATAA WAARABU

BAADA ya ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Yanga 0-0 Club Africain, mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika wawakilishi hao wa Tanzania kimataifa wanatarajiwa kusepa leo.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Waarabu hao wa Tunisia, Novemba 9,2022.

Wanahitaji ushindi wa aina yoyote ama sare ya kufungana ili wafanikiwe kutinga hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika.

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa wachezaji wanakiu ya kutafuta ushindi na malengo ni kusonga mbele kimataifa.

“Mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwani kushindwa kupata ushindi haina maana kwamba hatuwezi kupata matokeo.

“Kikubwa mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwa mechi ambazo tunacheza kwenye mashindano ya kimataifa bado wachezaji wana morali kusaka ushindi,”.

Previous articleKIPA KEPA KUIKOSA ARSENAL JUMAPILI
Next articleVIDEO:MWANAIDI AICHAMBUA YANGA ABAINISHA HATMA YA NABI