Home Uncategorized YANGA YAISHUSHA MTIBWA SUGAR, SASA NI NAMBA MOJA

YANGA YAISHUSHA MTIBWA SUGAR, SASA NI NAMBA MOJA

BAO la ushindi ambalo amefunga Feisal Salum mbele ya KMC limeishusha Mtibwa Sugar nafasi ya kwanza mpaka ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Fei amefunga bao hilo kwenye mchezo wa ligi uliokamilika kwa ushindi wa bao 1-0 KMC, Uwanja wa Mkapa.

Ni bao la nne la Fei ndani ya ligi na kuifanya Yanga kufikisha pointi 17 kibindoni huku Mtibwa Sugar ikibakiwa na pointi 15 kwenye ligi.

Ni dakika ya 80 bao hilo alifunga Fei kwenye mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Previous articleONGALA APIGA HESABU KUIKABILI SIMBA
Next articleMKWANJA MREFU SIMBA YAPATA KUTOKA M BET