Home Uncategorized SIMBA WABAINISHA WAMECHOKA KUFUNGWA NA YANGA

SIMBA WABAINISHA WAMECHOKA KUFUNGWA NA YANGA

UONGOZI wa Klabu ya Simba, umekiri kuwa umechoka kufungwa na Yanga, na safari hii watapambana kuhakikisha kuwa wanaibuka na ushindi katika mchezo wa ligi kuu leo Jumapili kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Simba wameshindwa kupata matokeo katika michezo minne iliyopita ambayo walikutana na Yanga, wakiambulia sare mbili na vipigo viwili, mmoja wakipoteza katika nusu fainali ya Kombe la Shirikisho huku wakifungwa pia katika mchezo wa fainali ya Ngao ya jamii.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema safari hii watahakikisha wanaibuka na ushindi mbele ya Yanga na hawatakubali kupoteza mchezo huo.

“Ni kweli tumeshindwa kupata matokeo mazuri mbele ya Yanga katika michezo ya hivi karibuni lakini niwahakikishie kuwa safari hii tutapambana kuhakikisha kuwa tunapata matokeo mazuri mbele yao Yanga, kila kitu ni mipango na mipango yetu ni kupata matokeo mazuri.

“Tunaye kocha mkubwa Juma Mgunda na tunao wachezaji wengi wazuri wenye uwezo mzuri na wataweza kutupa matokeo mazuri. Safari hii nawaambia kuwa tumechoka kufungwa na Yanga tupo tayari,”amesema.

Mchezo huo ni wa mzunguko wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara kwa watano hao kukutana leo Oktoba 23,2022.

Previous articleSERENGETI GIRLS WAPAMBANAJI WANASTAHILI PONGEZI
Next articleMABEKI YANGA KUMKAZIA MOSES PHIRI KWA MKAPA