Home Uncategorized AZAM FC KUIKABILI IHEFU

AZAM FC KUIKABILI IHEFU

 AZAM FC ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ihefu leo Oktoba 31.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex saa 1:00 usiku.

Azam FC itaingia uwanjani ikiwa imetoka kushinda bao 1-0 dhidi ya Simba na kusepa na pointi tatu mazima huku kipa wao Ali Ahamada akifanikisha ngome yao kutotikishwa.

Kali Ongala, Kaimu Kocha wa Azam FC amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo.

Kiingilio kwenye mchezo wa leo mzunguko ni 3,000 itakayowafanya mashabiki wa mpira kuona burudani kutoka Azam FC na Ihefu FC.

Previous articleTIKETI 10,000 MASHABIKI WA YANGA KUPEWA KUWAONA WAARABU
Next articleKELELE ZA MASHABIKI ISIWE SABABU WAAMUZI KUBORONGA