Home Sports KELELE ZA MASHABIKI ISIWE SABABU WAAMUZI KUBORONGA

KELELE ZA MASHABIKI ISIWE SABABU WAAMUZI KUBORONGA

KELELE za mashabiki uwanjani zina raha yake lakini hazipaswi kuwa kigezo cha kuwapa presha waamuzi kufanya maamuzi ambayo ni maumivu kwa wengine.

Kumekuwa na mwendo ambao haufurahishi kwa waamuzi kufanya maamuzi ambayo wanayajua wao wenyewe huku wakipewa shinikizo na mashabiki.

Hakuna suala hilo kwenye kazi hasa ambayo inasimamia taaluma ndani ya dakika 90 kikubwa ni kusimamia sheria 17 za mpira.

Pale ambapo inatakiwa kutolewa penalti itolewe kwa uhalali na pale ambapo hakuna penalti iwe hivyo kwani kila kitu kipo wazi na kinaeleweka.

Wasaidizi wa waamuzi ni muhimu kufanya ushirikiano mkubwa na mwamuzi wa kati kwenye suala la maamuzi kwani imekuwa tofauti kwa wakati huu kila mmoja anamtazama mwamuzi wa kati kuwa mwamuzi wa mwisho.

Kama utakumbuka wale waamuzi ambao walipewa tuzo ya seti bora ya wamuzi kwa msimu uliopita wa 2021/22 walipatikana kwenye mchezo walioonyesha ushirikiano ilikuwa Mtibwa Sugar dhidi ya Yanga.

Bao la Feisal Salum ambaye alifunga kwa kutumia mkono awali lilifutwa na hii ilitokana na ushirikiano kwa waamuzi hawa basi iwe hivyo kwenye mechi zote za ligi na Championship.

Kuboronga kisa mashabiki wanaimba ama wanapiga kelele haina maana muhimu maamuzi yazingatie kanuni na sheria 17 za mpira.

Previous articleAZAM FC KUIKABILI IHEFU
Next articleMECHI ZA KUAMUA NANI KUFUZU 16 BORA – UCL