
PRESHA YA UBINGWA IPO YANGA
NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga, amesema kuna presha kubwa katika kusaka ushindi uwanjani ambao utawapa ubingwa kutokana na kila timu kupiga hesabu za kuifunga Yanga. Yanga ni vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 36 kibindoni baada ya kucheza mechi 14, ndani ya ligi hiyohawajapoteza mchezo msimu huu, huku Jumatano ijayo wakitarajiwa kupambana na Ruvu Shooting. Akizungumza na Spoti Xtra, Nabi alisema: “Presha inakuwa kubwa hasa timu inaposaka ushindi,…