Home Sports SIMBA YAPATA TUZO,YAWAPOTEZA YANGA

SIMBA YAPATA TUZO,YAWAPOTEZA YANGA

LEO Juni13,2022 Klabu ya Simba imeweza kupewa tuzo yake baada ya kuwapoteza wapinzani wao wa jadi Yanga kwenye mchakato wa kura.

Ni Tuzo ya Klabu Bora kwenye Mitandao ya Kijamii Tanzania ambayo imetolewa na kampuni ya Serengeti Bytes.

Mbali na watani zao wa jadi Yanga pia Simba imeweza kuwashinda kwa kura Azam FC, Mbeya City, Ruvu Shooting.

Ni Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez akiongozwa na timu nzima ya kitengo cha habari inayoongozwa na Ahmed Ally huku mpiga picha akiwa ni Rubbi Hume waliweza kupokea tuzo hiyo

Previous articleYANGA KUMENYANA NA COASTAL UNION USIKU
Next articleFARID MUSSA AONGEZA DILI JIPYA YANGA