Home Sports FARID MUSSA AONGEZA DILI JIPYA YANGA

FARID MUSSA AONGEZA DILI JIPYA YANGA

FARID Mussa kiungo wa kazi ndani ya kikosi cha Yanga ameweza kuongeza kandarasi mpya kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Leo Juni 13,2022 Yanga wameachia picha ya nyota huyo akiwa na Injinia Hersi Said na kusindikiza na maneno haya:”Kiraka Farid Mussa bado yupoyupo sana,”.

Kiraka huyo bado yupoyupo ndani ya Yanga baada ya kuongeza dili jingine la miaka miwili.

Msimu huu amekuwa ana uhakika wa kuweza kuonyesha uwezo wake ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Nasreddine Nabi raia wa Tunissia.

Previous articleSIMBA YAPATA TUZO,YAWAPOTEZA YANGA
Next articlePUMZIKA KWA AMANI DAMIANO KOLA MZAZI WA RODGERS WA AZAM