Home Uncategorized YANGA KUMENYANA NA COASTAL UNION USIKU

YANGA KUMENYANA NA COASTAL UNION USIKU

 MCHEZO wa Yanga v Coastal Union unatarajiwa kuchezwa kesho, Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa timu zote mbili kuweza kuingia uwanjani kusaka pointi tatu.

Ikiwa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ikishinda mchezo huo basi inakuwa imeweza kujihakikishia lengo la kutwaa ubingwa wa ligi.

Vinara hao wa ligi kwa sasa wana pointi 64 kama wakishinda watafikisha pointi 67 ambazo hazitaweza kufikiwa na mabingwa watetezi Simba walio nafasi ya pili na pointi 51.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa usiku saa 2:30 utakuwa ni mchezo wa kwanza kwa timu hizi mbili kucheza muda huo kwa msimu wa 2021/22.

Coastal Union wao wapo nafasi ya 6 na pointi 34,katika mchezo wa kwanza Coastal Union ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0, Uwanja wa Mkwakwani.

Yanga inaendelea na mazoezi ambapo miongoni mwa wachezaji waliopo katika mazoezi hayo ni pamoja na Fiston Mayel,Jesus Moloko.

Previous articleRATIBA YA LIGI KUU BARA BONGO LEO
Next articleSIMBA YAPATA TUZO,YAWAPOTEZA YANGA