Home Sports GLOBAL FC YATOSHANA NGUVU NA BONGO MOVIES

GLOBAL FC YATOSHANA NGUVU NA BONGO MOVIES

TIMU ghali Bongo ya Global FC inayomilikiwa na Kampuni ya Global Group iliweza kuonyesha ubabe wake mbele ya timu ya Bongo Movie kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Shule ya Msingi Muhimbili jana.

Kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili ulichezwa mchezo mkubwa ambapo Global FC walianza kupata bao la kuongoza kwa shuti kali la Mbwana Junior akiwa nje ya 18 kwa pasi ya beki katili Omary Mdose.

Mdose kwenye mchezo huo upande wake ilikuwa ngumu kumpita jambo lililofanya lango la Mbuzi kuwa salama.

Iliwabidi Bongo Movie wacheze muvi ya kweli kwa kufunga bao la kusawazisha kwa penalti ya majaabu iliyofungwa na  staa wao Idrisa Makupa iliyomshinda kipa namba tatu wa Global FC, Issa Liponda, ‘Mbuzi’.

Kijiji kizima cha mastaa wa Bongo Movie walijitokeza kushuhudia mchezo huo ambao ulikuwa ni wa aina yake ikiwa ni pamoja na Mzee Chilo.

Nahodha wa Global FC,Wilbert Moland aliweza kutuliza presha ya wachezaji wa Global FC ambao walikuwa kwenye kasi kubwa kuwaandama Bongo Movie.

Mbali na mchezo huo pia Bongo Movie walikuwa na timu ya mpira wa mikono ambapo huko waliibuka mashujaa kwa ushindi wa mabao 10-1 Global FC.

Imeandikwa na Dizo Click.

Previous articleMCHONGO MZIMA WA AZIZ KI UMECHORWA NAMNA HII
Next articleRATIBA YA LIGI KUU BARA BONGO LEO