Home International CR KAFUNGA MWAKA KWA MABAO KIBAO

CR KAFUNGA MWAKA KWA MABAO KIBAO

MAISHA yake kwa sasa ya soka ni Saudi Arabia katika Klabu ya Al Nassr inayoshiriki  Saudi Professional League.

Ni Desemba 30, Al Nassr ilikipiga dhidi ya Al-Taawoun na kushinda mabao 4-1, kwenye mchezo wa ligi.

Katika ushindi huo wa Al Nassr, Ronaldo yeye alitupia bao moja dakika za lala salama kwa mpira wa kichwa.

Bao hilo linamfanya Ronaldo kufikisha jumla ya mabao 54 kwa ngazi ya klabu na taifa kwa mwaka 2023 ambao leo ndio unafikia kikomo hapo majira ya saa 5:59 usiku.

Idadi hiyo ya mabao inamfanya Ronaldo kuwa kinara wa mabao kwa mwaka huu akiwaacha akina Harry Kane mwenye mabao 52, Kylian Mbappe mabao 52 na Erling Haaland mabao 50.

Kupitia ukurasa wake wa kijamii CR 7 aliandika namba 54 kisha akadodnodhs ujumbe kuwa atasema ikiisha.

Previous articleMAELEKEZO YA MKWANJA BADO YAPO MERIDIANBET JUMAMOSI HII
Next articleMGHANA WA SIMBA KUTAMBULISHWA YANGA