Home Uncategorized SIMBA YAOMBA RADHI KWA MATOKEO MABOVU

SIMBA YAOMBA RADHI KWA MATOKEO MABOVU

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa kwa kilichotokea Februari 18, haikuwa malengo yao hivyo wanaomba radhi kwa mashabiki na Watanzania kiujumla.

Timu hiyo inayowakilisha Tanzania kwenye anga la kimataifa katika Ligi ya Mabingwa Afrika ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 0 -3 Raja Casablanca mbele ya mashabiki wao wakutosha.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa walikuwa wanahitaji ushindi lakini kilichotokea ni ukatili wa matokeo.

“Tulikuwa tunahitaji matokeo na mashabiki wengi walijitokeza kushuhudia burudani lakini kilichotokea ni ukatili wa mpira.

“Shukrani kwa mashabiki na wapenzi wetu. Klabu ya Simba inapenda kutoa shukrani za dhati kwa mashabiki waliojitokeza kwa wingi na kujaza uwanja, pia hata wale ambao hawakuja uwanjani.

“Tunawaomba radhi kwa matokeo. Tunaamini tumejifunza na tutaimarika kwa kufanyia kazi mapungufu kwani haya ni mashindano.

“Tunawaomba muendelee kuipa ushirikiano timu yenu kwani sisi Simba tunaamini kwenye nguvu moja kila kitu kitakuwa sawa,”

Previous articleYANGA YAITEMBEZEA KICHAPO TP MAZEMBE KIMATAIFA
Next articleKWANI MLISHINDWAJE? SIMBA YAWEKA REKODI MBOVU CAF