Home Sports RUNGU LILILOWAKUTA WAAMUZI NA DJUMA ACHA KABISA

RUNGU LILILOWAKUTA WAAMUZI NA DJUMA ACHA KABISA

NYOTA wa Yanga, Djuma Shaban amefungiwa mechi tatu na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Polisi Tanzania.

Mbali na kufungiwa mechi tatu pia ametozwa faini ya shilingi milioni moja kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Polisi Tanzania.

Mchezaji ambaye alionekana akipigwa kiwiko kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid alikuwa ni Yahya Mbegu na mwamuzi wa kati alishindwa kutoa adhabu kwenye mchezo huo.

Pia mwamuzi wa mchezo huo Hance Mabena wa Tanga yeye ameondolewa kwenye ratiba ya waamuzi kwa mizinguko mitatu kwa kosa la kushindwa kutafsiri sheria za mpira wa miguu kwenye tukio hilo la mchezaji wa Yanga.

Kwa kuwa Djuma alichezewa rafu kabla ya kulipiza tukio hilo.

Pia mwamuzi msaidizi namba moja Paschal Joseph kutoka Shinyanga na mwamuzi wa akiba Jackson Samwel wa Arusha wameondoewa kwenye ratiba ya waamuzi kwa mizunguko mitano kwa kosa la kushindwa kumsaidia mwamuzi wa kati katika kutafsiri vema sheria za mpira wa miguu kwenye tukio la Djuma.

Previous articlePABLO AKUTANA NA KITU KIZITO KUTOKA BODI YA LIGI
Next articleYANGA WAPIGA HESABU ZA USHINDI MBELE YA MBAO