Home Sports YANGA WAPIGA HESABU ZA USHINDI MBELE YA MBAO

YANGA WAPIGA HESABU ZA USHINDI MBELE YA MBAO

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba unawaheshimu wapinzani wao Mbao ambao watacheza nao leo kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 32 bora lakini watawafunga.

 Mkurugenzi wa Mashindano ndani ya Yanga, Thabit Kandoro amesema kuwa wanatambua kwamba wana mchezo mgumu ila wanahitaji ushindi.

“Baada ya droo kuchezwa tulijua kwamba tuna kazi ya kufanya mbele ya Mbao,tunawaheshimu wapinzani wetu lakini tunahitaji kuwafunga ili kuweza kusonga mbele.

“Kwenye mechi za mtoano timu itakayofungwa inatolewa hivyo kwa kuwa tunahitaji kutwaa Kombe la Shirikisho tunakwenda kucheza kwa nidhamu kwa kuwa tunawambua Mbao sio timu ya kubeza.

“Mchezo wetu dhidi ya Mbuni ulikuwa ni maalumu kwa ajili ya hesabu za mchezo wetu dhidi ya Mbao ambayo ni moja ya timu imara,” amesema.

Yanga mwaka 2021 iliishia hatua ya fainali na ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Simba, Uwanja wa Lake Tanganyika, mwisho wa reli Kigoma.

Jana Yanga imefanya mazoezi ya mwisho kabla ya kuvaana na Mbao leo Uwanja wa CCM Kirumba na miongoni mwa wachezaji waliopiga matizi ni pamoja na Chico Ushindi,Paul Godfrey,Fiston Mayele.

Previous articleRUNGU LILILOWAKUTA WAAMUZI NA DJUMA ACHA KABISA
Next articleVIDEO:UTAZAME UWANJA WA BUNJU COMPLEX ULE WA NYASI BANDIA